Ili kuweza kuangalia filamu na sehemu za tamthilia hapa Pendwa, unahitaji kuwa na vocha za kutosha kwenye akaunti yako.
Vocha za Pendwa SIO sawa na vocha za mitandao ya simu kama Airtel, au Tigo.
Sasa hivi vocha moja ni sawasawa na USD 1 au TZS 2,400/=. Sio lazima kununua vocha moja nzima. Kwa mfano, Vocha 0.25 zitagharimu USD 0.25 au TZS 600/=.
Filamu na sehemu za tamthilia nyingi hapa Pendwa zitakugharimu kiasi fulani cha vocha. Mfano, kwenye picha hapo juu, kukodi Season 1, Episode 3 inagharimu vocha 0.25 ambayo ni sawa na USD 0.25 au TZS 600/=.
Kujua vocha zilizobaki kwenye akaunti yangu
Kabla ya kukodi au kununua, utaweza kuona vocha ulizobakiwa nazo. Mfano, kwenye picha hapo juu, akaunti yangu ina vocha 2.5. Kukodi kipindi hicho kinagharimu vocha 0.25 kwa hiyo niko vizuri kuendelea. Kama vocha zangu zitakuwa pungufu basi itabidi nilipie ili niweze kukodi kipindi hicho.
Unaweza pia kwenda kwenye ukurasa wako wa "Settings" kuangalia vocha ulizobakiwa nazo. Ndani ya ukurasa huu, utaona mahali pameandikwa Credits. Hizo ndizo vocha zako zilizobakia.
β