Kwa wapenzi watazamaji wetu wanaotumia simu zenye mfumo wa Android kama Samsung, Tecno, Infinix na nyinginezo, unaweza kufuata maelekezo yaliyopo kwenye hapo chini ili kujiunga na Pendwa kwenye simu yako.
Je naweza kupakua application ya Pendwa Play Store? Kwa sasa hivi, bado tunafanya kazi kwa bidii kukuletea application yetu rasmi ya Pendwa ili uweze kuipakua moja kwa moja kwenye simu yako. Tutatangaza pale itakapokuwa tayari.
Ingia kwenye tovuti yetu https://www.pendwa.app/shows.
Gusa kitufe kilichoandikwa "GET STARTED / ANZA"
Sasa unaweza ukatengeneza akaunti yako kwa kupitia njia ya Google, Apple au Facebook kwa kubonyeza vitufe vinavyoonekana. Pia, unaweza kutengeneza akaunti yako kwa kutumia barua pepe (Email) na neno la siri (password).
Gusa kitufe kilichoandikwa "Create Account".
Mpaka hapa utakuwa umemaliza kutengeneza akaunti yako. Hongera sana 🙌👏. Kinachofuata sasa ni kutengeneza "Profile" yako utakayotumia kuangalia filamu na tamthilia hapa Pendwa. Kila akaunti inaruhusiwa kuwa na "Profile" hadi tatu. Kwa mfano, unaweza ukatengeneza profile mbalimbali kwa ajili ya rafiki na ndugu zako
Gusa kwenye sehemu iliyoandikwa "Account Holder".
Kwenye sanduku lililoandikwa "Name", ingiza jina la profile yako. Linaweza kuwa jina lolote lile.
Gusa kwenye kitufe kilichoandikwa "Choose Avatar". Hapa ndipo utaweza kuchagua picha (Avatar) itakayoambatanishwa na profile yako.
Baada ya kuchagua picha, gusa kwenye kitufe kilichoandikwa "Save".
Ukifika kwenye ukurasa huu basi utakuwa umemaliza kutengeneza profile yako. Hongera sasa aisee 😃. Gusa kwenye kitufe kilichoandikwa "Finish".
Ukurasa huu wa "Who's Watching" ndio utakaokuwezesha kuchagua profile gani unataka kutumia kuangalia filamu na tamthilia. Changua profile yako uliyoitengeneza hapo mwanzo. Unaweza kuichangua kwa kugusa picha yake.
Karibu Pendwa. Sasa utaweza kuanza kuangalia filamu na tamthilia kwa kutumia akaunti na profile yako uliyoitengeneza. Hongera na asante kwa kutumia Pendwa.
Video hii hapa chini inaingia kwa undani zaidi kuhusu kujiunga Pendwa.